
Head of Department
Idara ya Kiswahili inashughulikia somo la Kiswahili ambalo ni la lazima katika shule za msingi na za upili.Katika shule hii ya wasichana ya State house, walimu na wanafunzi hujikakamua vilivyo ili kuhakikisha kwamba ufanisi umepatikana.
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa elimu ya 8-4-4 , hakuna mwanafunzi aliyewahi kupata gredi ya E katika somo la Kiswahili.Mwaka wa 2015, matokeo ya Kiswahili yalikuwa 8.5 (Gredi B)
Shughuli za idara
a) Kuwafunza wanafunzi Kiswahili.
b) Kuwaandaa wanaunzi kwa mtihani wa kitaifa wa KCSE.
c) Kuwaandaa wanafunzi ili kushiriki katika mashindano na tamasha za muziki na maigizo.
d) Kuwashirikisha wanafunzi katika mijadala shuleni na kwingineko kama shule zingine,katika redio na runinga .
e) Kuwaelekeza wanafunzi katika utunzi wa kazi za Kiswahili kama mashairi, tamthilia na nyimbo.
f) Kuwahamasisha wanafunzi kuhusu matumizi ya lugha sanifu na kupambana na kilugha cha sheng’.

WALIMU KATIKA IDARA YA KISWAHILI
Idara hii ina waalimu wakakamavu na wanaojikakamua kweli nao ni;
a) Bi. Mungara -Mkuu wa Idara
b) Bi. Mvati- mwaklimu wa Kiswahili na mkuu wa idara ya ushauri na maelekezi.
c) Bi. Barasa -Msaidizi wa Mkuu wa Idara
d) Bi. Kinuthia -Mwalimu wa Kiswahili
e) Bi. Nabukhwesi – Mwalimu wa Kiswahili
f) Bi. Mboya- Mwalimu wa Kiswahili
g) Bwana Indindi – Mwalimu wa Kiswahili.
LCHAMA CHA KISWAHILI
Idara ina chama cha Kiswahili kinachoongozwa na Bi. Barasa .Wao hushiriki katika majadiliano na sanaa za Kiswahili.Wanafunzi husajiliwa wanapoingia kidato cha kwanza.
MALENGO
• Kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi shuleni anaongea lugha sanifu.
• Kuinua gredi ya somo la Kiswahili hadi gredi ya A.
CHANGAMOTO
• Mawasiliano kwa lugha ya sheng’ miongoni mwa wanafunzi.
• Imani potovu kuwa Kiswahili ni lugha ngumu .
• Wanafunzi hawadwusu Kiswahili kama wafanyavyo masomo mengine hasa sayansi.